Rais wa Tanznia John magufuli ametimiza ahadi yake ya kumpa mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta tausi wanne . Rais Kenyatta aklikabidhiwa zawadi hiyo siku ya ijumaa na balozi wa Tanzania humu nchini Pindi Hzara Chana . Akizungumza baada ya kupokea ndege hao rais Kenyatta alimshukuru Magufuli akisema ndege hao wanaashiria umhimu wa upendo ,umoja na undugu kati ya Kenya na Tanzania .
Magufuli alikuwa amemwahidi rais Kenyatta kwamba nangempa tausi hao kama zawadai wakati Kenyatta alipomtembelea kwa ziara ya kibinafsi ya siku mbili mwezi uliopita . Alifanya utani kwamba pindi tu rais Kenyatta alipokanyaga katika boma lake ,alianza kuwatamani tausi hao ambao pia walionekana kumfurahia .Magufuli, hata hivyo alisema kwaba iwapo ndege hao watazaana ,basi Uhuru anafaa kuwarejesha wanne Tanzania .