Aiaga dunia baada ya kunywa lita 5 za chang'aa

KIMRAID0304D
KIMRAID0304D
Mashindano huwa ni kitu kizuri maishani. Jamaa, ndugu na marafiki wanaposhiriki katika mashindano huwa ni wakati mzuri wa kujistarehesha na huwa ni fursa ya kutangamana. Kisa kimetokea jumapili iliyopita katika kitongoji duni cha kaunti ya Bungoma wakati ndugu na jamaa walikutana kushiriki katika mashindano ya ulevi.

Soma mengine hapa:

Katika kikundi hicho, alitokea jamaa na kibuyu cha lita 5 za pombe na noti ya shilingi moja mkononi.

‘Atakayemaliza pombe hii nitamkabidhi shilingi elfu moja,” aliwaeleza marafiki zake.

Mwendeshaji bodaboda alitokea na kwa ujasiri akachukua kibuyu hicho cha chang’aa na kumaliza pombe yote. Dakika chache ata kabla apewe zawadi yake kuu ya elfu moja ,alianguka na akazirai. Marafiki wenzake walimbeba hobelahobela na kumpeleka nyumbani kwake. Alionekana mnyonge na kupumua kwa nguvu sana.

Soma hapa:

Marafiki wake walimwacha apumzike na siku ilyofuata wakafika kumwona na kumjulia hali mwenzao. Cha kustaajabisha ni kuwa walimpata ameiaga dunia kwani hakuna mtu angemsaidia katika chumba kile. Kwa mujibu wa taarifa za vyanzo vinavyoaminika,pombe aliyoikunywa ilimzidia na kumfanya afariki.