Aina ya chakula unafaa kula ili kupunguza uzito - Jennifer mwangangi

jennifer mwangangi
jennifer mwangangi
Jennifer Mwangangi ambaye ni daktari wa maswala ya lishe, ukipenda nutritionist.

Swala ambalo Jennifer ameamua kuzingatia kwa kina zaidi ni jinsi binadamu anaweza fanya ili kumuezesha kupunguza uzito, haswa wakati huu ambapo visa vya magonjwa ambayo husababishwa na uzito vimeongezeka.

Kulingana na Mwangangi mbali na mazoezi, wakenya wapaswa kuangalia chakula wanachokula na pia ambao wana nidhamu ifikapo maswala ya lishe, pia wapaswa kujua kuwa mazoezi ni muhimu sana.

Alitaja sukari kama mojawapo ya viini ambavyo huchangia pakubwa ongezeko la uzito mwili, na kuwa shauri wakenya kukoma tabia ya kula sukari kwa wingi.

Watu wanapaswa kujua sukari inachangia ongezeko la uzito mwilini na sukari hiyo inapatikana katika vyakula tunavyo kula kila siku. 

Kwa hili naongelea chochote kinachotengenezwa na sukari kwa mfano chapati na mandazi. Anasema Jennifer.

Unajua utafiti unaonesha kuwa mtu wa kawaida hula vijoko 42 vya sukari kila siku na ujue unapaswa kula vijiko kumi pekee kwa siku.

Anasema kuwa chakula kingi ambacho huja katika boxi hatufai kula kwani chakula kizuri ni kile kimetoka shambani moja kwa moja.

Kitu kingine kinacho ongeza uzito ni pombe. Pombe yeyote sio bora lakini wine sio mbaya yaundwa na zabibu lakini hupaswi kunywa kupindukia.

Kingine ni maziwa kwani ya siku hizi sio mzuri kama kitambo, maziwa nzuri ni ya mbuzi au ngamia. 

Mbali na chakula, Jennifer anawashauri watu kuwa homoni pia ni jambo la muhimu na kila mmoja anapaswa kujua hali ya homoni zake.

Anaongeza kuwa homoni ya insulin husaidia kupigana na sukari mwilini na kupeleka sukari ile kiunoni. Aliongeza kuwa mwili ukitoa Insulin kwa wingi basi inaweza sababisha ugonjwa wa kisukari.

Nahimiza watu wale chakula chenye fibre nyingi na hizo zapatikana kwa chakula ambazo zimetoka kwa shamba kwani husaidia sana na kusaga chakula kwa haraka.

Mfano wa chakula hizi ni mboga, matunda, mihogo na viazi vitamu.

Je ni chakula kipi ambacho watu wanao jaribu kupunguza uzito wanapaswa kula?

Watu wawachane na mchele au wali, ugali ule wa unga wa kusaga, chapati wale nusu na iwe ile ya unga wa kahawia (brown).