Ajabu! Kiranja wa shule kumchapa mwanafunzi hadi kifo kwa ajili ya Biblia

Mwanafunzi aliripotiwa kuaga dunia baada ya kuchapwa na kiranja wa shule alipompata akisoma bibilia katika shule ya upili ya St Joseph Nyabigena kaunti ya Kisii.

Ni mtindo ambao umetoka kwa wazai hadi kwa watoto, kwa hivo watoto hao wanaiga mfano huo kutoka kwa wazazi.

Mwanafunzi huyo alitangazwa kufariki punde tu alipofikishwa katika hospitali ya misheni ya Tabaka alipopelekwa baada ya tukio hilo, mwanafunzi aliye ongea kuhusu kisa hicho.

Alisema kuwa kiranja huyo wa kidato cha nne aliweza kumsamba/kumpiga kofi mwanafunzi huyo kisha kumchapa mateke katika tumbo yake mara kadhaa.

Mhathiriwa huyo ndiye alikuwa mvulana katika familia hiyo, aliweza kujiunga na shule hiyo kwa utu wa msamaria mwema anaye mlipia karo ya shule baada ya kumpoteza mama yake 2015.

Ingawa utawala wa shule ulikataa kuongea na vyombo vya habari baadhi ya walimu wa shule hiyo wamelaumu usimamizi wa shule hiyo kwa kuwapa viranja mamlaka mingi.

Kamanda wa kaunti hiyo Martin Kibet aliweza thibitisha kisa hicho na kusema kuwa polisi wanafanya uchunguzi zaidi.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Nyarambe waliweza kuwachunguza na kuwauliza walimu maswali bali hawajaweza kufanya hatua ya kuwakamata washukiwa wowote.

Ripoti zinasema kuwa mwalimu kuu wa shule hiyo Mathew Simiyu aliweza kuita wanafunzi kwenye gwaride na kisha kuwashauri waweze kutulia na kisha akatoka kwa haraka na kuenda.

Wanafunzi waliweza kukataa chakula cha mchana na kuanza kuandamana kwa ajili ya kisa hicho huku walimu akisema watakao husuika wataadhibiwa.

Wazazi waliofika katika shule hiyo waliambia vyombo vya habari kuwa waliweza kuzungumzia jambo hilo katika mkutano wa wazazi mara nyingi.

Hii ni kuhusu viranja kupewa mamlaka ya kuwaadhibu wanafunzi wenzao.