Ajali ya ndege, Wilson Airport - Nairobi

Ndege
Ndege
Ndege ya shirika la Silverstone Air imeanguka katika uwanja wa Wilson jijini Nairobi. Ndege hiyo ya abiria 60 ilipotea njia ilipokuwa inajiandaa kupaa angani na kuanguka Ijumaa mchana.

Ilikuwa inajiandaa kwa safari kuelekea mjini Mombasa ilipopata matatizo ya kimitambo kabla ya kupaa angani. Abiria kadhaa wamepata majeraha madogo.