Aki Mulee Nataka Kijana Wako Jeff, Naskia Baridi! Dama Wa Donholm Afungua Roho (AUDIO)

Bali na usafiri wake, kicheko chake na kipawa cha kucheza na kufunza kadanda, Ghost Mulee anajulikana kuwa baba hodari wa vijana wawili barobaro; Carl na Jeff ambaye ndiye kifungua mimba.

Mara kwa mara bwana Mulee hukumbana na wanadada wengi ambao kupitia Radio Jambo na mitandao ya kijamii hutangaza nia yao ya kuoa Vijana wale kwani hukiri ni watanashati kupindukia.

Basi kama baba, Mulee ambaye huwapatanisha mabibi na mabwana, huwa hana budi ila kuwatetea vijana wake huku akidai kuwa wako shuleni au ni wachanga sana na basi hawako tayari kuingia katika ndoa.

Asubuhi ya leo mtangazaji huyo alikuwa na kibarua kigumu wakti alipokumbana na mwanadada mmoja ambaye alitaka sana kumjulia mmoja wa vijana wale, Jeff hali.

Kulingana na mwanadada huyo kwa jina Damaris almaarufu 'Dama kutoka Doni', alikiri kuwa anampenda sana kijana yule licha ya kuwa hajawahi patana naye, na kuwa yuko tayari kuwa mpenzi wake.

Isitoshe, Dama ambaye amemshinda Jeff kiumri (Dama 24, Jeff, 18 ) alifungua roho akisema anaumia sana kwani baridi imemzidia na hana la kufanya.

"Mulee aki sasa nitapata aje Jeff, aki usicheke ninaumia, Umsalimie."  Alisema Dama kabla kuarifiwa kuwa Jeff yuko shuleni kwa sasa.

Ako shulee? Aki mimi nataka kumuona aki mimi naumia namtaka...usikate simu Gidi nataka uchukue number yangu. Mimi nina miaka 24 nataka mnitafutie hapo juu mimi naskia baridi!" Aliongeza Dama huku akiwamaliza watangazaji hao kwa kicheko.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be