Akothee amtunuku shabiki hela kibao, amtaka asaidie wanyonge

Screenshot_from_2019_12_31_10_27_33__1577777275_21228
Screenshot_from_2019_12_31_10_27_33__1577777275_21228
Staa wa muziki wa kizazi kipya nchini Akothee amemtunuku shabiki wake elfu 30 kwa mapato anayopata kupitia mtandao wa YouTube.

Emmanul Onu alituzwa hela hizo kwa kutaja nyimbo zote alizowahi kuimba Akothee.

Akothee alikuwa amefanya hakikisho kwenye mitandao ya kijamii kuwa atakayefanya hivyo atamtuza.

https://www.instagram.com/p/B6sC7OMnsEL/

 Aidha, Akothee alimtaka mshindi huyu kuwajibika katika kuwasaidia wanyonge katika jamii.

"Muda mfupi ujao nitamzawadi mshindi wa YouTube, swali langu kwa mshindi wa KSh30,000 utakayopokea kutoka kwangu hii leo, uko tayari kuchangisha kiasi kwa wasiojiweza? Utatujulisha endapo utatajwa, hauhitaji kuwa milionea kupeana," alisema Akothee.

Akothee amehusika sana katika vitendo vya usamaria wema na kutoa msaada mkubwa kwa wasiojiweza katika jamii hususan wakaazi wa kaunti ya Turkana.

Baa la njaa lilikuwa limegumbika eneo hili na kulihitajika usaidizi wa dharura zaidi ndiposa akatoa msaada huo.

Wengi walimsifia zaidi kwa tendo la kuwajali watu wa tabaka la chini katika jamii.

Msanii huyu aidha alianzisha mpango madhubuti wa kuwasaidia wasiojiweza na familia zilizoathirika kutokana na ukame eneo hilo.