Akothee apendezwa na urembo wa wanawe Massawe Japanni

Kwa kweli urembo sio kitu kigeni katika familia ya mtangazaji Massawe Japanni, urembo wake na umaridadi umetiririka hadi kwa wanawe watatu wa kike.

Kitu kimoja anacho tambulika nacho Massawe ni urefu, weusi, afya na umaridadi wa nywele yake na kwa kweli tunda halianguki mbali na mti kwani sifa hizo hizo ndizo zina watoto wake.

Wikendi iliyopita, mtangazaji huyo wa Bustani la Massawe, pamoja na wanawe waliamua kujiburudisha kwa kupiga picha kama familia huku urembo wao ukiwavutia mamia ya wakenya pamoja na watu mashuhuri.

Mmoja wao ni msanii na rafikiye Massawe, Akothee, ambaye anatambulika kama rais wa wanawake au kina mama ambao hawajaolewa.

Baada ya kuchapisha picha zao katika mtandao wa Instagram, Akothee kama tu mashabiki wengine walimezea mate nywele za kina dada hao na hakusita kutoa maoni yake.

Alionesha kupendezwa kwake na zile nywele huku akijihurumia kwa kuwa yeye hana nywele ndefu na isitoshe yeye hubidi ameshonwa nywele za kuongeza, al maarufu weave.

Alisema,

Nywele na mimi napambana na weave 😭😭😭

Tazama picha za Massawe Japanni na wanawe.