Akothee asimulia aliyoyapitia na kisha kuwa mwanamziki maarufu

index
index
Akothee almaarufu Esther Akoth ni mama wa watoto watano na pia ni muimbaji wa Kenya ambaye ameenea sana katika uimbaji wake.

Mwanamziki huyu amekuwa mjasiri baada ya kupitia maisha magumu,aliolewa akiwa miaka 14 kisha akaenda ng'ambo alipofukuzwa akiwa na mimba ya mtoto mtoto wake wa nne.

Akizungumza na Massawe Japanni, Akothee alieleza shida alizo pitia.

Mzungu alimwambia arudi Afrika kwa sababu alikuwa anahitaji mtoto bali si bibi ilhali Akothee alikuwa anahitaji bwana.

Mzungu alimpata mwanamziki huyu katika mji wa Mombasa Shanzu alipokuwa akipika katika hoteli yake pia alikuwa akiwauzia watu pombe na hapo ndipo mzungu alimualika waende Switzerland.

"Niko na shida ya Fallopian tube. Nilipata shida hiyo baada ya kumzaa kitinda mimba wangu. Niliambiwa nifanyiwe oparesheni wakati huo huo niliweza kumpigia mume wangu ili akuje atie sahii.

Hii ni baada ya kuwapigia wazazi wangu simu lakini zilikuwa mteja ndipo nilipompigia mume wangu lakini akani kana,"Akothee alisema.

Baada ya mzozo huo Akothee na mumewe Jared waliweza kukosana; yaani mapenzi ya Akothee ilikwisha wakati huo wa tatizo hilo.

"Mume wangu aliponiambia 'dont call me again telling me those nonsense'nilianguka nikazirai.

Nilipoamka nilikuwa na alama ata hii alama iko tumboni napenda kuionyesha kwa maana inanipa sababu nyingine ya kuishi. Nilipopona nilimpeleka kortini kwa maana nilikuwa nasumbuka na watoto peke yangu nilikuwa nataka anisaidie.

Lakini alikuja na kijitabu kikubwa ilikuonyesha hawawezi saidia mtoto ata mmoja. Hapo ndipo nilijua nilikuwa na haribu wakati na masaa yangu bure."aliongezea Akothee.

Pia Akothee ameweza kumsaidia kijana Ziky kwa mziki wake na pia ana mpango wa kumfungulia biashara ili aweze kujikimu kimaisha.

Ziky na Akothee washaatoa ngoma ya kwanza iitwayo 'Basi'.

Akothee alianza kama dereva wateksi mjini Mombasa. Aliweza kutumia nafasi aliokuwa nayo vizuri.

Pesa za mwanamuziki huyo kupitia njia ya kucheza muziki uliomwezesha kwenda ng'ambo na kulipwa laki 3 ambazo alikuja kuwekeza kwa nyumba kisha akanunua gari ya KAT516F ili kuanza maisha nayo.

"Niliweza kutengeneza sabuni na kuzungusha kwa mahoteli. Mume wangu aliponinyag'anya watoto sikuweza kuwachukua tena bali nili tuma ndugu yangu awaendee.

"Usiku nilikuwa dereva wa teksi na mchana na tengeza sabuni na kuzungusha mitaani,"Akothee alisema.