Akufaaye kwa dhiki: Kutana na rafiki wa chanda na pete wa Jacque Maribe

jacque
jacque

Hivi karibuni, Jacque Maribe amekuwa akionekana katika mitandao ya kijamii ya watu mbalimbali na hivi juzi, alionekana katika mtandao wa kijamii wa Stephen Letoo

Stephen Letoo ni mtangazaji wa Citizen Tv na rafiki yake Jacque Maribe ambaye alibaki naye ata wakati ambao alikuwa na kesi yake na aliyekuwa mpenzi wake Jowi.

Wawili hawa,Stephen na Jacque walikuwa katika mkahawa wa Roadhouse iliyo mtaaa wa Kilimani.

Marafiki hawa walipiga picha na alipoiweka kwenye mtandao wa kijamii,Stephen aliandika,

Each friend represents a world in us, a world possibly not born until they arrive, and it is only by this meeting that a new world is born.

Kwa wale wasiojua, Stephen Letoo ni mmoja wa rafiki zake Jacque Maribe ambao walielewa fika methali isemayo akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki kwani Jamaa huyu hakumuacha Jacque bali aliendelea kuwa rafiki yake na kumsaidia awezavyo.

Mbali na Stephen Letoo, rafiki yake Jacque wa karibu ni Dennis Itumbi.

Rafiki wengine wa Jacque ni; Mwanamziki Kambua ambaye walikuwa wakifanya kazi pamoja,Muthoni Wa Mukiri ambaye hufanya kazi katika televisheni ya Inooro,Terryanne Chebet na Kirigo Ngarua ambao walikuwa wakifanya kazi pamoja.
Shix Kapienga naye ndiye rafiki yake Jacque wa kufa kupona.

Kitu ambacho Jacque alifahamu siku ambazo alikuwa na shida ni kuwa kuna rafiki wa kweli na wale ambao si wa kweli.