Al Shabaab

Al shabaab wateka nyara madaktari 2 wa Cuba

Wanamgambo wa kundi haramu ya Al shabaab wamevuka mpaka na kuwateka nyara madaktari wawili kutoka nchi ya Cuba katika mji wa Mandera mapema leo.

Inaaminika kwamba madaktari hawa walizuiliwa barabarani na waasi hawa huku wakiwafyatulia risasi walinzi wao na kuangamiza mwanapolisi mmoja.

Afisa mmoja wa polisi aliweza kutoweka na kukwepa mauti huku wanamgambo hao wakiwachukua madakari hawa na kuhepa nao hadi nchi jirani ya Somalia.

Hali ya madakatri hawa waliotekwa inasalia tete na ya hofu kwani haijulikani walipo. Vikosi vya usalama vinachana mbuga kuwatafuta wahalifu hawa na kuwaokoa mateka.

Kundi hili limekuwa mwiba hapa nchini hususan kaskazini mwa nchi. Ni mapema mwakani walipovamia maeneo ya burudani na kujistarehesha ya Dusit hapa jijini Nairobi.

 

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments