Alaa! Kwani wamerudiana? Maribe na Omondi wajivinjari

Jacque Maribe aliyekuwa mtangazaji wa Citizen TV na mcheshi Eric Omondi wameonekana pamoja zaidi ya mara mbili sasa. Wiki zilizopita, Jacque Maribe na baba ya mtoto wake, Eric Omondi walihudhuria sikukuu ya kuhitimu kwa mtoto wao na kwa sasa wawili hawa wanajivinjari pamoja na mtoto wao.

Mashabiki wengi wa Jacque Maribe wamekuwa na mwaswli mengi kwani hawajui kati ya Jowie, Itumbi na sasa Omondi ni nani mpenzi wake Jacque.

Baada ya Jacque kufunguka kuhusu baba ya mtoto wake, ameonekana akizuru maeneo mbali mbali akiwa na baba ya mtoto wake.

Wiki hii, wawili hawa pamoja na mtoto wao na mwanamziki Awilo Logomba walienda mtaa wa Emayian Luxury Camp maeneo ya Masai Mara ili kujivinjari.

Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, Eric Omondi aliweka picha zake wakiwa pamoja na Jacque kwenye Jacuzzi iliyokuwa na maua ya waridi.

Wawili hawa wameonekana kuwa wako sawa pamoja na si ajabu wamekuwa pamoja kwa muda mrefu.

Maskini Jowie alikuwa anatamani sana kumfanya Jacque awe mke wake lakini kwa sasa bado ako gerezani anakula kiapo chake.

Je mambo yatakuwa vipi au Jowie atasaidiwa vipi?

Tazama picha na usisite kuorodhesha maoni yako kuhusu wawili hawa!