Alazwa;Ndugu wa Jose Chameleon amelezwa hospitalini baada ya kuvamiwa

NA NICKSON TOSI

Ndugu wa msanii Jose Chameleone kwa jina  Pius Mayanja almaarufu kama  Pallaso amelazwa hospitalini katika taifa la Afrika Kusini baada ya kuvamiwa na genge la watu linalosemekana kupigana na vita dhidi ya ubaguzi almaarufu kama xenophobic.

Katika video iliyokuwwa kwenye mtandao wake wa Facebook,msanii huyo alisema kuwa walikuwa wanaendesha gari na rafikiye kabla ya kuvamiwa kwa upanga,mawe,na fito zito .

Akitokwa na machozi ,Plalaso alielezea jinsi alivyoebuka kifo chake baada ya ku[pigwa hadi kupoteza fahamu.

Pallaso amesema kuwa hana ufahamu wowote wa alipo rafikiye kwa jina Kiwunya Fred kwa sababu alimwacha kwa gari alipokuwa anajaribu kuponya maisha yake.

“They beat me up real bad. I fell down, I was stabbed. As I tried to run I was hit by a car. I tried to ask for help from the owner of the car but he just drove off so I kept running with people chasing me with machetes. They pulled my hair and beat me up. Xenophobia is real. I am not sure I’ll leave this place alive because I’m still in hiding. Am currently hiding in a garage at a school. Please pray for me, I need help,” Alisema Pallaso.

Pallaso amekuwa Afrika kusini kwasiku kadhaa akishugulikia tamasha mbali mbali na kurekodi nyimo mpya .

Alhamisi, uongozi wa kampuni inayommiliki iliandika ujumbe wa kudhibitisha kitendo hicho na kuwashukuru mashabiki wote waliomuombea Pallaso .

“Thank y’all our Fans Worldwide for the concern and prayers 🙏🙏🙏 We would like to inform you that our artist PALLASO has been located and rescued and at the Hospital however his condition is still very bad keep him in your prayers 🙏🙏🙏🙏A Big Thank Mc Norman for the support and to the South African High Commission for also following up on this 🙏,” Ulisoma ujumbe.