Alexis Sanchez yuko tayari kubakia ugani Old Trafford

Mshambulizi wa Manchester United na chile, Alexis Sanchez yuko tayari kubaki ugani old Trafford na kubigania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza kulingana na mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskajear.

Ole amesema kuwa mshambulizi huyo yumo kwenye mipango yake ya msimu huu na sasa anamtarajia kucheza mechi nyingi kuliko alivyofanya msimu uliopita.

Sanchez alicheza mechi 45  tangui ajiunge na Manchester United huku akicheka na nyavu mara tano kwenye mechi hizo.

"Alexis ni mchezaji wa hali ya juu sana. Anafanya mazoezi yake vyema sasa na nafikiri kuwa yeye anataka kuwa mmoja wa kikos chetu hapa msimu huu. Kwa sasa yumo nyuma kiasi kwa sababu ya match fitness lakini ndani ya muda mchache atakua sawa kabisa kuvalia jezi ya Manchester Tena," Ole Gunnar alisema.

Mlindalango wa kabu ya Liverpool,Adrian huenda asishiriki mechi ya wikendi dhidi ya Southampton. Adrian alipata jeraha kwenye mechi ya UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea. Mkufunzi wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa mlinda lango huyo alipata jeraha akshanglia baada ya ushimdi.