Ali Kiba afunguka mwanzo mwisho sababu ya kumtishia Diamond

Ali Kiba na Diamond Platnumz wamekuwa na vurugu nyingi kati yao. Vurugu ambayo tunaamini ni kwa sababu ya kimziki na si mambo mengine.

Vita vya hivi juzi vilikuwa baada ya Ali Kiba kukataa kuenda kwenye shamra shamra za Wasafi Festival na timu yote ya Wasafi pamoja na wanamuziki wa bongo walibaki wameduwaa baada ya mwanamuziki huyu kukataa mualiko huu.

Zaidi ya hayo, kuna wakati ambao wawili hawa walirushiana maneno kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Ali Kiba akisema kuwa Diamond alikuwa anafanya mambo kama mtoto wa kidato cha pili. Salaale!

Katika mahojiano ya hivi juzi na Times FM, Ali Kiba alisema,

‘Kilichofanya ni post nitoe taarifa ni kwa sababu waandishi wa habari walikuwa all over wanapiga masimu. So kile kitendo ili niweze kustopisha wengine nikaona nipost ili wasione kama waandishi wa habari nimewakosea heshima sipokei simu zao ama nawadharau. I had to do that. Heshima kila mtu tunaamua tu kuwekeana heshima kwa sababu sipendi kumzungumzia mtu kwa mabaya wala ningependa kumzungumzia mtu kwa mazuri. Vile vile sidhani kama ilikuwa sawa katika kila event zao wanihusishe. Mimi siko tayari na wanajua kabisa I cannot do it na I’ve told them before nikamwambia fanya wewe, mimi nitakuja kufanya ya kwangu. Walikuwa wanatafuta namna gani waweze kubeba ile attention