Alice Wahome amtaka Emmanuel Wangwe kuelezea ni kwa nini ametumiliwa kwa kamati ya bunge

Mbunge wa Kandara Alice Wahome sasa anamtaka kiranja wa wengi katika bunge la Kitaifa Emmanuel Wangwe kumfahamisha ni kwanini alitimuliwa kutoka kwa kamati ya haki na sheria ya bunge la kitaifa.

Katika barua ambayo mbunge huyo ameiandika ,amemtaka Wangwe kmfahamisha njia mwafaka ambazo zilichukuliwa ndiposa akatimuliwa kutoka kwa kamati hiyo.

Barua ya Wahome inajiri muda mfupi tu baada ya mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kutangaza rasmi kujiondoa kwa kamati ya Uchuguzi wa Umma bungeni.

Chama tawala cha Jubilee kimekuwa kikifanyia mabadiliko idara kuu katika mabunge yote mawili haswa kwa viongozi ambao wamekuwa wakiegemea upande wa naibu rasi.