Alichokisema babake kuhusu mauaji ya Monica Kimani,Jowie ni mhusika mkuu

Monica-kimani-family-696x465
Monica-kimani-family-696x465
Babake marehemu Monica Kimani bado anazongwa na fikra.

Kifo cha kutatanisha cha bintiye hadi leo kinamfanya kuwa na masimango akilini.

Paul Ngarama ambaye ni mhubiri amefunguka jinsi familia inapitia wakati mgumu.

Paul ameambia waumini wake wamwombee katika hali hii ngumu.

Kesi ya mauaji ya Monica bado inaendelea ili kubaini mahasidi waliomuua.

Jowie na mwanahabari Jacque Maribe ni washukiwa katika kesi hii.
Jowie ambaye anafahamika kama Joseph Irungu anatuhumiwa kuwa mhusika mkuu
Mshukiwa huyu amezuiliwa katika rumande jela kubwa ya Kamiti na amekuwa akitokeza mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.
Kwa mujibu wa washahidi, Jowie alikuwa mtu wa mwisho kuonekana na marehemu Monica Kimani.
Lee Omondi, rafiki wake Monica aliambia jaji James Wakiaga kuwa alitembelea nyumba yake Septemba 19,2018.
Nia na azma ya kufika kwake ilikuwa kuchukua stakabadhi alizokuwa nazo marehemu.

"Nahitaji maombi yenu.Kesi ya binti wangu Monica ilianza hii wiki. Kuna uamini kwa uwezo mkubwa wa farasi na majeshi makubwa ila mimi naamini Mungu..." Alisema babake Monica.
Mwili wa Monica ulipatikana umetupwa katika bomba la maji chumbani Kilimani.
Koo la mfanyabiashara huyu wa miaka 28 ilikuwa imepasuliwa, mikono kufungwa, kinywa chake kufungwa na nguo zake kuraruliwa.