Katika posti Insta, Otile amesema kuwa yoyote anaweza chezea nywele za mrembo wala sio miguu.
Haya yanajiri baada ya wawili huwa kurudiana na kuwa sawa katika mahusiano.
Kwa kile kinachokisiwa kuwa kiki, wawili hawa walitengana kwa tuhuma za Otile kuchepuka.
”Gusa nywele zake na nitakasirika sana. Ila ukitaka kuona nimekasirika zaidi hebu gusa miguu yake, ndio kiungo cha mwili ninachokipenda. Nafikiria kuikatia bima...' Alichapisha Otile.
Hii ni ishara kuwa janja janja za Otile zimemnasa mrembo huyu.
Hii ni baada ya meseji kuvuja zikionyesha mawasiliano yake na mabinti wengine.
“Kitu moja nakifahamu kabisaa ❤️ YOU GIRL @NABBI,” OB alichapisha.
Mwanadada kwa jina Peggy alishukiwa sana katika kuchochea penzi la wawili hawa kuota mbawa.
Peggy hatimaye alikana taarifa hizi katika mahojiano na tovuti ya Mpasho.