Alichokisema Rashid Abdalla baada ya mamake kupata afueni

Screenshot_from_2019_12_28_11_53_02__1577523202_17545
Screenshot_from_2019_12_28_11_53_02__1577523202_17545
Mwanahabari wa kituo cha runinga cha Citizen Rashid Abdalla amejawa na furaha tele baada ya kuona mamake anapata nafuu kutokana na hali yake ya ugonjwa.

Katika taarifa za awali, Rashid alieleza kutokuwa na amani moyoni baada ya mamake mzazi kutatizika kiafya.

"Si rahisi na haitakuwa rahisi lakini Ishallah Mungu atakuwa nawe. Kuwa mvumilivu na mwenye nguvu," alisema Rashid kwa mamake.

Kupitia mtandao wa Insta, mwanahabari huyu alichapisha picha za mamake na kuomba wafuasi wake kumsaidia katika maombi.

Akimtaja kama nguzo imara katika maisha yake, Rashid ametoa shukrani kwa Mungu katika hali hiyo ngumu.

"Mama kwa mwanawe, mtoto kwa mamaye..." Aliandika Rashid.

https://www.instagram.com/p/B6i-qwIBFT-/