Alikiba amchokoza Diamond kwa kufichua anavyompenda 'baby mama' wake Hamisa katika video mpya

Alikiba  na Hamisa Mobetto  wameutoa wimbo mkali ambao sasa unatesa masafa katika mitandao  .

Video hiyo ya wimbo ‘Dodo’’ inaeleza hafla ya harusi  huku Hamisa akiwa ndiye mhusika mkuu katika masimulizi ya wimbo huo .

Itakumbukwa kwamba Ali kiba na Diamond  wana bofu ambayo imekuwa wakati mwingine inazima na kulipuka na

ni kinaya kwamba Hamisa naye ni 'baby mama' wa Diamond kwani walikuwa wapenzi awali na wana mtoto. Katika wimbo huo, Ali Kiba anaeleza jinsi anavyompenda Hamisa(Hatujui Simba atasemaje kuhusu hilo)

 “Kupenda ni vitendo si maneno maneno, leo nakupa kitengo kwa kufika Malengo, umeziba Mapengo, kwa upendo upendo, Bora wanazengo anze vikao vya sendoff Eeeh, Maa’ inashuka mistari hiyo

Anaongeza Kiba ;

‘Maana we mrembo nakujuzaaah..mama nashukuru umekuza, chanda kama pete nitakutunza … na umeshanizimaa, ayoyoyooo Love, ayoyoyooo my love, ayoyoyooo Love, your love, Dodo langu Beibe,”  Ali Kiba anafoka mistari hiyo katika wimbo wenyewe

Mashabiki wengi walionekana kumsifia Kiba kwa kuamua kumtumia Hamisa katika video ya wimbo huo

presenterdmike “Hakika @hamisamobetto ameitendea haki Video ”

ridhonekigu_ ‘King of tanzania   big up bro ”

lumiere_mbilizi ‘Ye baba! Afu nimemuona @hamisamobetto ndo imenoga zaidi…”

officialgerard_hero ‘Huu Unyama wa mama DAYLAN NOMA  Sijui Itakuaje kule  ”

ally__kiba “Hii Video haijawahi tokea hapa Tanzania tangu dunia iumbwe sasa mtu ukibisha ruksa kunya boga ama tikiti #DODO Video link on bio!!… ”

c.g.englibert ‘Shkamoo baba…. kupenda Ni vitendo si maneno maneno :