‘Mwajiri wangu alinitaka nifanye mapenzi na mbwa wake.’ Mkenya aliyekwenda Bahrain kufanya kazi asimulia masaibu yaliyompata

Visa vya  wakenya kuteswa katika nchi za mashariki ya kati wanakoenda kufanya kazi  wakati mwingine vimezua hamaki na huruma kutoka kwa wakenya.

Lakini baadhi ya  mambo wanayopitia wasichana wa Kenya katika nchi hizo ni ya kushangaza. Baadhi ya mateso hayo huwaacha waathiriwa na   makovu ya kimwili ilhali wengine huvurugwa vibaya kiakili na kuhitaji msaada wa ushauri.  Jessica Ndanu* alifaulu kurejea Kenya baada ya miaka mitatu ya mateso huko Bahrain na imemchukua miaka miwili kutaka kuzungumzia kuhusu kilichomfanyikia akiwa huko. Mateso ya mwajiri wake yalikuwa mtindo wa maisha lakini kamwe hatosahau siku ambayo  mtoto wa kiume wa mwajiri wake alipomvua nguo na kisha kumtaka afanye mapenzi na mbwa wao kwenye balcony huku akiitoa simu yake ili kuchukua video hiyo.

Tukio hilo lilisalia katika fikra za Ndanu na alipofaulu kurejea Kenya, hakuwahi kutaka kuzungumzia hilo na siku hiyo aliponea kwa  tundu la sindano wakati mbwa aliyefaa kumvulia nguo alipoonekana kutojali kilichotakiwa kufanyika. Ndanu anasema baada ya kupitia mateso kwa mwajiri mmoja, aliweza kuhamishwa hadi kwa mwajiri mwingine kumbe alikuwa katoka kwenye pani na kujiingiza katika kaa zima la moto.

‘Kwa mwajiri wangu wa kwanza, ningeosha jumba zima la ghorofa tatu kuanzia juu hadi chini na ingenichukua karibu saa nne kumaliza. Nilianza kuumwa na mgongo na wakati mwingi nilikuwa nikitumia dawa za kutuliza maumivu’ anasema Ndanu

Anasema mtindo huo wa kazi ngumu uliendelea kwa miezi minane tangu alipotoka Kenya na kaanza kutamani kurejea nyumbani lakini pasipoti yake ilikuwa imebanwa na ajenti aliyempeleka kwa kazi hiyo. Alipougua na kisha kulalamika kuhusu kazi nyingi alizokuwa akipewa,  Ndanu alifaulu kuhamishwa kwa mwajiri mwingine ambako masaibu ya kutakiwa  kufanya mapenzi na mbwa yalimpata. Mwajiri wake mpya alikuwa na wake wawili na Ndanu alikuwa miongoni mwa walofanya kazi katika nyumba zote. Mke wa kwanza alikuwa na watoto wakubwa ambapo wanawe wawili wa kiume walikuwa wakatili na wakati mwingine wangewalazimisha waafrika wanaofanya kazi kwao kuwaosha miguu wanapocheza video games.

‘Kilichoshangaza ni kwamba wazazi wao hata hawakujali kuhusu ukatili na tabia za wanao. Waliangalia kana kwamba kila  mambo waliofanya yalikuwa ya kawaida’.  Anasema Ndanu

Ndanu alivumilia yote kwa sababu alivyokumbuka mateso ya kukosa kazi Kenya na jinsi alivyomuacha mamake na mtoto wake wa miaka mitatu, kurejea nyumbani mikono mitupu halikuwa chaguo kwake.

Anasema uamuzi wake wa kutaka kurejea Kenya ulishika kasi  baada ya tukio hilo ambapo alipomaliza kufanya  kazi zote na kwenda katika makaazi ya wafanyikazi, aliagizwa kurejea katika jumba kuu la mwajiri wake. Mwanawe alikuja amebeba kijibwa chake na akiwa ameandamana na rafiki zake. Walionekana  kuwa na hila ya kutaka kufanya jambo baya lakini hakujua ni nini walichotaka. Muda mfupi baadaye  walimuelekeza kwenye balcony ambako mwanawe mwajiri wake alimtaka avue nguo abaki uchi. Ndani alifikiri alitaka kumchapa kwa kiboko cha mpira ambacho walikuwa wamezoa kuwachapia wafanyikazi.

Alipovua nguzo zake, hakuchapwa bali mmoja wa  rafiki za mtoto wa mwajiri wake alikiachilia kile kijibwa na kukipa maagizo ya kumsongea Ndanu. Hapo ndipo alipogundua walichotaka kuona kwa sababu walianza kuzitoa simu zao kuchukua video ya kilichofaa kufanyika lakini kwa bahati nzuri, kile kijibwa hakikuwa na  haja wala ufahamu wa kilichotakiwa kufanya. Walioneana kukasirishwa na hilo na kumfurusha Ndanu kutoka pale lakini macho yao yakimuonyesha kwamba watajaribu tena uovu huo wakati mwingine.

Siku chache baada ya tukio hilo, Ndanu alimuambia ajenti wake  kwamba alikuwa mgonjwa na alitaka kurejea Kenya haraka iwezekanavyo. Kwa bahati nzuri, hapakuwa na pingamizi na wiki moja baadaye alikuwa amerejea Kenya. Miaka miwili baadaye, Ndanu yungali hajasahau ukatili ambao nusra ungeyavuruga maisha yake kabisa.