'Alikuwa anataka kulipwa ili ahudhurie EP launch yangu,'Tanasha afichua kwanini Diamond alihepa EP launch

Hatimaye Tanasha Donna alifichua kwanini msanii Diamond Platnumz hakuweza kuhudhuria EP launch yake iliofanyika mapema mwaka huu, mkutano huo ulifanyika katika eneo la Sarit Centre Expo mjini Nairobi.

Akiwa kwenye mahojiano Tanasha alisema kuwa Diamond hakuhudhuria mkutano huo wakati wa mwisho kwa maana hakuwa amelipwa chochote.

"It’s was a lot to do with when business and love meet, it was an issue with the management in terms of payment, and a whole lot of things behind it. It was more business related as to why he decided not to show up last minute. (I was supposed to pay him to show up at the EP Launch).” Alizungumza Tanasha.

Alizidi na kuzungumza;

"Nilikuwa tayari nafanya kile niwezalo na timu yangu, ni ukweli timu yangu ni ndogo lakini ina bidii kama ya mchwa, tulifanya chote tuliweza

Tulitoa pesa zetu mfukoni, tulipambana tulialika kila mtu katika kila kona lakini mambo mwishowe hayakufaulu, kama mnavyojua Diamond si msanii wa kualikwa mahali na pesa kidogo

he is quite expensive. So it was a whole back n forth with the management and a whole lot of stuff, and I don’t blame them it’s their business I respect their business at the end of the day, so I’m not putting the blame on anybody, none of them."Tanasha Donna alisema.

Siku hiyo hiyo Chibu Dangote aliwafahamisha mashabiki wake kuwa alirudi mjini Tanzania kwa ajili jambo la dharura lilitokea.

“Kutokana na tatizo la ghafla lilotokea nyumbani, imenibidi niruke Dar es Salaam Maramoja kwajili ya kulisolve....hivyo naweza fika nimechelewa, au pengine kutofanikiwa kuhudhuria ghafla ya Uzinduzi maalum ya EP ya Mpenzi wangu Mjini Nairobi Usiku wa leo...Niwakumbushe tu kuwa Event hio itakuwa inaruka live kupitia ...Mlio majumbani msikose kutazama.” Aliandika Diamond.

Mkutano huo uliudhuriwa na wasanii kama;Nameless, Khaligraph Jones, Wahu, Bahati, Romy Jons, Jacqueline Wolper, Shaffie Weru, Kevin Obia, Juma777, Eric Omondi, Antonio the MC, Weezdom, Simon Kabu, Sarah Kabu, H_art the Band, Quadrah Nizar, Shaq the Yungkin, Barak Jaccuzi, Olive Karmen, Sean Andrew, Nviiri the Storyteller, Diana Marua, Nadia Mukami, Phoina na wengine wengi.