'Alikuwa shoga! Alionioa kuwafumba watu macho...’ Mwanadada asimulia yaliyomkumba

Ameeleza tukio la kushangaza mwanadada mmoja ambaye amejitambua kama  Fidi  katika mitandao ya kijamii kuhusu jinsi alivyoolewa na mwanamume ambaye alikuwa shoga. Baada ya kuanza  uhusiano walipokutana huko Malindi wakati wa  likizo ya krisimasi, Fidi  alimpenda jamaa huyo ambaye baadaye alimtambulisha kwa wazazi wake na wakafanya sherehe ya ndoa ya kitamaduni .

Hata hivyo, shauku yake ilipanda zaidi wakati waliporejea bara, Eldoret na mume wake kuanza kufanya ziara za kushtukiza kurejea Pwani bila kueleza sababu za kuridhisha za ziara zake hizo .  Mwanzoni alikuwa akisema kwamba alikuwa akienda kazi lakini Fidi alifahamu kwamba kazi yake ilikuwa ya  afisa wa mifugo na  alishangaa ilikuaje hadi akalazimika kwenda Malindi kila mara bila notisi .

Alipokuwa akienda Malindi, mume wake alikuwa akikatiza mawasiliano kabisa na ilikuwa vigumu kufahamu alikuwa eneo lipi hasa na alichokuwa akifanya. Siku moja Fidi alimuuliza kuhusu safari hizo na ndiposa ukweli ukadhihirika . Mume wake hakuwa na soni  bali alimuambia kwamba alikuwa mpenzi wa jinsia moja a wakati akienda malindi , alikuwa akikutana na raia wa kigeni ambao pia walikuwa wapenzi wake. Fidi alivunjwa moyo kufahamu pale kwamba mume  wake alikuwa kahaba wa kiume na kwanza kahaba wa jinsia moja .

Mume wake aliendelea kujitetea akisema kwamba alimuoa ili kuwafumba watu macho na kuepuka maswali ya jamaa na rafiki zake waliokuwa kila mara wanampa presha ya kupata mke .  Mume wake alimuambia kwamba starehe zote walizokuwa wakizipata na yale maisha mazuri zilifadhiliwa na wazungu waliokuwa ‘wakifanya mapenzi’ naye na hivyo basi alikuwa na chaguo la kusalia katika ndoa yao au kuondoka na kukosa yote ‘mazuri’.

Fidi alichanganyikiwa asijiue kuomboleza  hatua ya kufumbwa macho na mapenzi au ugunduzi kwamba aliolewa na mtu ambaye hakuwa na nia ya kumchukulia kama mke bali kama  chombo cha kuficha   alichokuwa akifanya. Hatimaye aliamua kujipa  muda nje ya ndoa ili akitaraji kwamba mume wake angeweza kubadilika na kuachana  na wapenzi wale wa kiume ili waanze upya maisha yao .