‘Alinipiga matiti pasi ndio wanaume wasiniangalie’ Asimulia ‘utamaduni’ wa Cameroun aliofanyiwa na shangazi yake

Utamaduni au mtindo wa kupiga matiti pasi ili kuyazuia yasiwe makubwa umekithiri afrika magharibi na hasa nchini Cameroon . Wanaotekeleza  hilo hudai kwamba hatua ya kuzuia kukua kwa matiti ya wasichana wanaoanza kubaleghe huwazuia kuwavutia wanaume na hivyo basi kuepuka dhulma za kimapenzi lakini  jambo hilo limetajwa na wanaharakati kama ukiukaji wa haki za wasichana na dhulma kwa waathiriwa.

Kabla ya masimulizi ya  Jane  Mbithi mwenye umri wa miaka 32 sasa kuibuka, wengi nchini  hawana ufahamu iwapo kuna utamaduni kama huo. Jiwe hutiwa motoni kama kaaa kisha kupitishwa juu ya matiti kwa lango la kuyapunguza. Jane alifanyiwa  utataribu huo  miaka 18 iliyopita  na shangazi yake ambaye alikuwa Mtawa(Nun) na alikuwa akiishi Cameroun wakati huo . Alipokuja nyumbani kwa likizo alimpata Jane akiwa ameanza kubaleghe na matiti yake yameanza kujitokeza, yakionekana kupitia nguo yake. Shangazi yake hakufurahia hilo na mara moja akamuambia mamake jane kuhusu  hatari ya mwanawe kubakwa na wanaume na hivyo basi kuliwa na haja ya kuyapunguza matiti yake. Mamake alishangaa  hilo litafanywaje lakini shangazi yake kwa ajili ya kuwa mtawa aliheshimiwa sana pale bomani na kila alichosema kilikuwa sheria. Alieleza jinsi utaratibu huo utakavyofanywa na muda sio mrefu, kila jane alikuwa akivumilia takriban dakika 20 za uchungu wakati jiwe la moto lilipokuwa likiwekwa kifuani mwake ili kupunguza kiasi cha matiti yake .

Wenzake shuleni walishangaa mbona alikuwa akilia wakati wote na kushika kifua chacke kwa uchungu. Wengine kama  rafiki yake wa karibu Stella alishangaa mbona  hawakuwa wakioga pamoja kama awali bila kujua kwamba Jane alikuwa akificha  alama katika kifua chake na kupungua kwa matiti yake kwa ajili ya uovu aliokuwa akifanyiwa na shangazi yake kutumia mila aliotoa Cameroun .

Alipokuwa msichana  mkubwa kujiunga na  chuo kikuu, Jane alijipata na matatizo ya kujiamini kwa sababu alijiona na kujihisi tofauti kama wasichana wenzake. Wengine walikuwa wakimfanyia mzaha kwa kumuita ‘mvulana’ kwa sababu ya kukosa matiti bila kujua masaibu aliyopitia . Jane hakuweza kumchukulia hatua yoyote shangazi yake kwa sababu uamuzi huo pia ungemuingiza taabani mamake ambaye alikuwa  amekubali  afanyiwe utaratibu huo . Walimuambia wakati huo kwamba kila wanachofanya ni kwa manufaa yake bila kujua athari za kitendo  hicho katika maisha yake  ya baadaye .

Nchini Cameroun ambako utamaduni huo umekithiri, serikali na mashirika mbalimbali ya haki za binadamu yanapambana na  uovu huo ili kuzuia mateso kwa maelfu ya wasichana. Kupiga matiti pasi ni zimwi kama utamaduni wa kuwakeketa wasichana katika baadhi ya jamii za humu nchini. Athari za kitendo hicho kwa Jane hazitaisha hivi karibuni na zinamuathiri hadi wakati huu katika maisha yake ya utu uzima .