Alitoka kwa lebo ya Alikiba, akaingia kwa lebo ya Harmonize. Ibraah atisha na ngoma mpya TZ

EWbgbJxWAAAB-uT
EWbgbJxWAAAB-uT
NA NICKSON TOSI

Ni wiki moja imepita tangu msanii chipukizi kutokea Tanzania kwa jina Ibraah kutangaza wazi kuwa amesitisha mkataba wake na lebo iliyokuwa inamilikiwa na Alikiba. Ibraah akitoa uamuzi huo alimsifia pakubwa Alikiba akisema alimpatia fursa ya kipekee ambayo wengi walikuwa wamemnyima mara ya kwanza na kuongezea kuwa uhusiano wake na Kiba utakuwepo kwa miaka.

Baada ya kujiunga na lebo inayoongozwa na Harmonize kwa jina Konde Music Worldwide, Ibraah amewadia na bonge la hiti ambalo limetajwa kuwa litaleta mshawasha mkubwa sana Tanzania .

Tazama wimbo wenyewe huu hapa.

Je Ibraah atafana kama bosi wake Hatrmonize anavyotesa kwa sasa?