Aliyefariki kutokana na corona Bomet azikwa usiku

Wakaazi wa kaunti ya Bomet wakiwa katika harakati za kuhakikisha kuwa wanafika kwa nyumba kabla ya makataa ya serikali kufikia, gari aina ya Land Rover lililokuwa limebeba mwili wa mgonjwa wa virusi vya corona lilikuwa linaelekea katika kijiji cha Kagawet, lokesheni ya Itembe katika eneo bunge la Chepalungu kumzika mwathiriwa huyo usiku.

Mkuu wa afya katika kaunti hiyo amesema Erick Kosgei wa miaka 55 alisema mwendazake alipumzishwa kulingana

Baadhi ya jamaa zake waliokuwa hawajatangamana na Kosgei kabla ya kufariki walirushusiwa kuhudhuria mazishi hayo huku wengine waliojumuika naye wakiwekwa kwenye karantini.

Hafla hiyo ilifanyika mida ya saa 7 jioni chini ya dakika chache mno.

Picha zilichukuliwa na jamaa walioshuhudia mazishi hayo zilionyesha jamaa waliokuwa wamevalia nguo nyeupe wakiwa wanaendesha hafla hiyo.

Kosgei yadaiwa kuwa alikuwa na ugonjwa wa kisukari kabla ya kukumbana na mauko yake.

Watu takriban 36, wakiwemo 16 wa familia yake wamewekwa kwenye karantini ili kubaini iwapo walioambukizwa virusi hivyo baada ya kujumuika na mwendazake.