Aliyekuwa gavana wa Vihiga Moses Akaranga kuwania urais wa FKF

moses akaranga
moses akaranga
Aliyekuwa gavana wa kaunti ya Vihiga, Moses Akaranga amejiunga rasmi katika kinyang'anyiro cha urais wa shirikisho la soka nchini FKF kabla ya uchaguzi utakaofanyika mwaka ujao.

Hatua hio imewakanganya wajumbe wa eneo la Magharibi kwani kuna wagombea wengine wawili ambao wameonyesha nia ya kugombea.

Aliyekua mwenyekiti wa tawi la shirikisho hilo huko Magharibi Andrew Amukowa na aliyekua naibu katibu mkuu wa muungano wa makocha Khamisi Shivachi wote kutoka eneo hilo pia wanawania wadhfa huo.

Klabu ya Gor Mahia itarejea mazoezini leo tayari kwa mechi yao ya ligi dhidi ya Chemilil sugar katika mechi ya KPL kesho.

Gor walirejea nchini Jumatatu usiku kutoka Algeria ambako walipoteza 4-1 na USM Algiers katika raundi ya pili ya mchujo ya ubingwa bara Afrika.

KO’gallo watakua na kibarua kigumu kwani lazima wawanyuke USM mabao 3-0 ili kufuzu kwa awamu ya makundi.

Timu ya voliboli ya kinadada itaendeleza juhudi za kupata ushindi hii leo watakapochuana na Brazil katika michuano ya kombe la dunia, inayoendelea nchini Japan.

Kenya haijapata ushindi wowote na wanavuta mkia kwenye kipute hicho, baada ya kupoteza mechi zao dhidi ya Marekani, Uholanzi na Serbia.

Kocha mkuu Paul Bitok anasema morali iko juu kwenye kambi baada ya kinadada hao kupokea marupurupu yao kutoka kwa wizara ya michezo. Bitok anaamini wanaweza kushinda angalau seti moja dhidi ya miamaba hao wa Amerika Kusini licha ya ujuzi wao.