Aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana akamatwa

mungatana
mungatana

Aliyekuwa mbunge wa Garsen Danson Mungatana siku ya Jumanne alikamatwa na maafisa wa DCI katika hoteli moja mjini Nairobi.

Munagatana alipelekwa katika makao makuu ya DCI kuhusiana na madai ya kupokea pesa kwa njia ya udanganyifu.

Soma habari zaidi;

Mfanyibiashara aliyekuwa amempa pesa alishuku wakati alipoitishwa pesa zaidi  na kupiga ripoti kwa polisi.

Mkutano kisha ulipangwa katika hoteli moja mjini Nairobi ili wakutane na ni hapo ambapo Mungatana alitiwa mbaroni pamoja na mwanamume mwingine kwa jina Collins Waweru, aliyekuwa amesema ana uwezo kufanikisha makubaliano baina ya Mungatana na mfanyibiashara huyo.

Soma habari zaidi;

Mwaka jana mwezi Aprili, Mungatana alikuwa miongoni mwa washukiwa 26 walioshtakiwa katika mahakama ya Malindi kwa madai ya kupokea shilingi milioni 51 kwa njia ya ufisadi.

Maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi walimkaamata Mungatana baada ya kuvamia boma lake mjini Nairobi.