Nahashon Mutua

Aliyekuwa OCS wa Ruaraka Nahashon Mutua kuhukumiwa kifo

Ni mauaji ya kikatili ambayo yamekuwa yakitendeka kote nchini.

Aliyekua OCS wa Ruaraka Nahashon Mutua amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mwanabiashara wa Miraa 2013.

Polisi waliniweka pilipili katika sehemu zangu za siri – Judy Wangui

Jaji wa mahakama ya juu Stella Mutuku Alhamisi alisema kuwa mahakama imeonyesha kesi yake zaidi ya shaka yeyote.

Nahashon mutua
              Nahashon Mutua

Alisema kuwa Martin Koome alipokea matibabu ya kiunyama na hakuna shaka yoyote kuwa Nahashon ndiye alisababisha kifo chake.

Koome alisema kuwa kuna mmoja mdogo atakaye sema kuhusu kufiwa kwa familia dhidi ya uchungu uliosababisha kifo cha mwana familia wao.

Patanisho: Bibi yangu amenuna na tunazungumza kupitia watoto wetu

“Kukubali na wakati ndio utapona uchungu wao, ni dhahiri kuwa kifo cha Koome kimeweza chukua mtu ambaye alikuwa anawakimu na mwenye alikuwa anashughulikia mahitaji yao, ukweli huu umeweza kubadilisha maisha yao kabisa,” Alisema jaji stella wakati wa utawala wake.

Mutua ameweza kupewa siku,14, ili kufanya rufaa katika utawala huo wa jaji wa mahakama ya juu Stella Mutuku.

Katika utawala wa mahakama ya juu mwaka jana ulimpata Mutua akiwa na hatia ya kumuua Koome, aliye kuwa mahabusu katika kituo cha polisi cha Ruaraka.

milimani.law.courts.history(2)

Alijaribu kumuekelea Kevin Odhiambo ambaye pia alikuwa habusu katika kituo hicho na kisha kuachiliwa baadaye.

Koome alikuwa mwanabiashara wa kuuza miraa katika eneo la Baba ndogo, Ruaraka kaunti ya Nairobi.

Koome aliweza kurudi kwake nyumbani akiwa mlevi baada ya kazi kisha kuanza vita na mke wake, ndipo aliweza kuwapigia polisi simu ili waje wamshike Koome.

Jambazi aliye nusurika kutoka mikononi mwa wakazi wa Taita Taveta

Mashtaka iliweza kuonyesha mahakama vile Mutua alienda kwa urefu ili kuzuia haki kutendeka, kwa kupeana hongo ya millioni moja na hata kujaribu kumuekelea Kevin kwa kitendo hicho.

Hii ndio kesi iliyo katika mstari wa kwanza polisi ambaye ni OCS kupatikana na hatia ya mauaji yasiyo na hatia. Hii itakuwa funzo kwa watu au walaghai ambao wanawauwa wananchi wasio na hatia kiholelaholela.

 

 

Photo Credits: Collins Kweyu/the star

Read More:

Comments

comments