Aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe aaga dunia

Habari zinazochipuka sasa hivi ni kuwa aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amefariki.

Mugabe ambaye ndiye alikuwa rais wa kwanza wa Zimbabwe baada ya nchi hiyo kujinyakulia uhuru, aliaga asubuhi hii ya leo akiwa na umri wa miaka 95.

Mugabe alishikilia usukani wa Zimbabwe kwa miaka 37.

Kifo chake Mugabe chaja wiki chache tuu baada ya picha yake kusambaa mtandaoni kwa mara ya kwanza, zaidi ya mwaka mmoja tangia kung’atuliwa kwake uongozini.

Picha hiyo ilichapishwa na mwanawe, Robert Mugabe Jr katika mtandao wake wa Instagram, huku hali ya afya yake ikionekana imedhoofika.

Kwa picha hiyo, uso wake Mugabe ulionekana umebadilika kupindukia, huku amekalia gari la gurudumu akipunga hewa na mwanawe.

 

-BBC