Allan Wanga astaafu soka la kimataifa

Mshambulizi wa timu ya Kenya Harambee stars na Kakamega Homeboyz,Allan Wanga amestaafu kucheza mechi za kimataifa.Wanga alitoa habari za kustaafu kake kwenye mtandao wake wa instagramu.Kwa sasa, wanga anakichezea Kakaemga homeboyz mjini kakamega.

"Ni wakati wangu sasa kuwaachia wachezaji wengi nafasi kuitumikia taifa letu kama nilivyolitumikia mie. Naitakia Harambee stars heri njema kwenye michuanio itakayoshiriki. Sasa nabadilika na kuwa shabiki nambari moja wa staas. Asanteni sana FKF na wakenya kwa kunishabikia. # DaimaMkenya."

Allan wanga aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii.

Wanga alichezea Kenya mechi 44 huku mechi yake ya kwanza ikiwa ni mwaka 2007 dhidi ya Nigeria. Kwenye mechi hizo, Wanga amewaamsha mashabiki mara 22 kwa kucheka na nyavu. Goli lake la kwanza lilikuwa mwaka 2008 kwenye mchuano wa CECAFA dhidi ya Tanzania.