Aliongeza kwamba alikuwa kiongozi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Nairobi mwaka wa 1987 na aliteswa mwaka huo na vyombo vya usalama nchini kwa kujihusisha na shughuli a kisiasa .Miguna Miguna amesema hakusafiri kwa hiari kwenda Canada kutoka Kenya na hajawahi kuukana uraia wa Kenya . Serikali ilimtimua Muguna nchini mwaka jana kwa madai kwamba alipewa paspoti ya Kenya kinyume cha sheria .
“ Wakati Miguna alipopewa paspoti ya Kenya kinyume cha sheria alikuwa akifanya kazi katika afisi ya waziri mkuu kama mshauri wa Raila Odinga’ ilisema taarifa ya serikali .Miguna ameipuuza taarifa hiyo ya serikali akisema kwamba alilazimika kukimia mafichoni kwa sababu ya hofu ya uwezekano wa kushtakiwa na hakuondoka Kenya kwa hiari. Amesema maafisa hao 25 wa serikali waliiharibu paspoti yake na vifaa vyake kabla ya kumfurusha kwa lazima nchini bila notisi yoyote .