Size 8; Mama mkwe amekuwa nguzo yangu

sNA NICKSON TOSI

Size 8  na Dj Mo wamekuwa wakiposti picha zao jinsi wanavyoishi maisha yao katika mitandao ya kijamii lakini kitu ambacho wapenzi hao wawili wamekuwa wakiweka mbali na mitandao ni baadhi ya jamaa zao wa karibu ambao hawajawahi kutuma picha zao katika mitandao yao.

Hivi maajuzi, Size 8 aliamua kuwaacha wengi vinywa wazi baada ya kutuma picha ya mama mkwe wakiwa pamoja katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii.

Size 8 alimsifia mama huyo kwa kile alisema amekuwa na yeye kwa mazuri na mabaya na kila wakati amekuwa akimshauri endapo wametofautiana na mumewe.

"Namshukuru kwa kuwa nguzo muhimu maishani mwangu, siwezi kulipa mchango wake ambao amenifanyia ila Mungu ambariki kwa yote aliyonitendea," Aliandika Size 8.

Size 8 alimpoteza mamake mzazi kutokana na matatizo ya figo,  siku chache tu kabla ya kujifungua kifungua mimba wao Ladasha Wambo.

Baada ya kutundika picha hiyo ya mamamkwe kwenye ukurasa wake, mashabiki walikuwa na haya ya kusema.

ndiemanicholas Hapo ndo kuwa quarintine sasa

jamsbrawn97 Nimepatana na mama wambo na mukurino mmoja wakiwa wamebebwa na mafarasi

knic_k_nacks Aaaawww❤️❤️❤️

Mhariri; Davis Ojiambo