Amepatikana: Jinsi Diamond hujitetea kila anapopatikana na mipango wa kando

Diamond (1)
Diamond (1)

Mwanamziki Diamond amejulikana kwa usanii wake uliokolea na hata pia tabia yake ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mabinti wengi.

Diamiond naye, si mchache kwani kila wakati apatwapo akiwa na mpango wa kando, yeye hujitetea vilivyo na ni vigumu sana kutoamini anachosema.

Tazama uongo Diamond husema kila wakati apatikanapo na wapenzi wake akiwa na mpenzi mwengine.

  1. Zari

Diamond alikuwa na mpango wa kando alipokuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama wa watoto wake wawili.

Staa huyu alipoulizwa kilichomfanya afanye kitendo kama hiki alisema kuwa, mke wake alikuwa anaishi Afrika Kusini na yeye Tanzania na kwa hivyo hawakuwa wanaweza kushirikiana kimapenzi mara kwa mara.

Katika mahojiano kitambo kidogo, Diamond alisema kuwa, ni yeye alimkosea sana mke wake Zari kwani, Zari alikuwa mwanamke mzuri sana aliyependa familia.

''THROUGHOUT MY RELATIONSHIP WITH ZARI, I WRONGED HER MORE THAN SHE WRONGED ME. SHE WAS SMART, SHE WAS A WIFE MATERIAL THAT I CAN ASSURE.'' Diamond alisema.

Vilevile, Diamond alisema kuwa kilicho wafanya wakate uhusiano wao na mke wake ni kutokutana mara kwa mara na iwapo anatamani kushiriki na mke wake kimapenzi hakuwa anaweza.

''WHAT I CAN SAY LED TO US INTO SPLITTING WAS THE DISTANCE AND LACK OF  CONSTANT ENGAGEMENT WITH EACH OTHER.''

I’M STILL YOUNG AND I’M A STAR. WOMEN ARE ALWAYS DROOLING OVER ME. IMAGINE, I LEAVE THE OFFICE, I GO HOME AND I DON’T GET MY LOVER, SHE IS IN SOUTH AFRICA. I WILL ENDURE THIS FOR ONE OR TWO WEEKS AND THEN GIVE UP.''

2. Wema Sepetu

Wema Sepetu ambaye alikuwa mpenzi wake Diamond alisema kuwa, hata ikiwa Diamond ataachana na yote na arudi kwake kumposea, haezi kubali.

“EVEN IF DIAMOND DECIDED TO DROP EVERYTHING AND PROPOSE TO ME, I’D NEVER ACCEPT HIS PROPOSAL,” alisema.

Diamond alipokuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu alifanya uhusiano wa kimapenzi na rafiki wa dhati wa mpenzi wake, Bi Jokate Mwegelo

3. Jokate Mwegelo

Jokate na Diamond walikuwa na uhusianio wa kimapenzi kabla ya binti huyu kupendana na Ali Kiba.

Akizungumzia uhusiano wake na Jokate Mwegelo, Diamond alisema kuwa binti huyu hakuwa na kosa lolote kwani ni yeye alitaka uhusiano wa kimapenzi na binti huyu na kisha baadae akamwacha ili amrudie Wema Sepetu.

''JOKATE WAS VERY INNOCENT AND NEVER DID ANYTHING WRONG TO ME.

I PUT HER THROUGH A LOT OF TROUBLE AND CREATED A PERCEPTION IN PEOPLES MIND THAT SHE WAS A BAD GIRL WHO HAD SNATCHED ME FROM WEMA

TRUTH IS I’M THE ONE WHO PURSUED HER. I DATED HER THEN BROKE UP WITH HER WITHOUT A REASON AND RAN BACK TO WEMA.'' Diamond alisema.

4. Penniel Mungilwa ‘Penny’

Penny Na Diamond walifanya uhusiano wao wazi mwaka wa 2013 baada ya kukata uhusiano wake na Wema Sepetu.

Kabla ya wapenzi hawa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, Diamond alihusiana kimapenzi na binti huyu huku Wema Sepetu akiwa mpenzi wake.

Ushirikiano wa kimapenzi wa Diamond na Penny haukukaa kwa muda mrefu kwani Diamond alimwacha binti huyu na kurudi tena kwa Wema Sepetu kabla kumwacha na kumpata Zari Hassan.

Diamond ambaye ana uhusiano wa kimapenzi na binti wa kutoka humu kenya Bi Tanasha Donna, alisema kuwa anampenda sana bitni huyu na hatakuwa na mpango wa kando.

''ROHO YANGU MIE. NAKUPENDA MPAKA NAKUPENDA SANA. NAJUA WANASUBIRI LINI…ILA WATASUBIRI SANA! SIKUCHEAT HATA IWEJE.'' Diamond alisema.
Hata hivyo tukizingatia yaliyowafika waliokuwa wapenzi wake Diamond, tunaomba tu alichosema Diamond ni ukweli na kuwa atakuwa mwaminifu kwa mpenzi wake Tanasha Donna.

Je ni sababu zipi ambazo mpenzi wako amewahi kujitetea nazo ulipompata na mpango wa kando?