massawe ilikuaje

Ilikuaje :Niliteswa kwa kupigwa na mke wangu-James Njenga asimulia masaibu yake

Kwa mwanamme kujitokeza wazi na kukiri kupigwa na mkewe hasa hapa afrika ni jambo kubwa kwa sababu jamii inawahitaji wanaume kuvumilia kila aina ya ugumu wa kaisha .Lakini kwa James Njenga ,hatua yake kujitokeza na kukiri kupitia kipigo na mateso  ya mke wake ni jambo la ujasiri ambalo anasema linalenga kuwazuia wanaume kuteseka katika ndoa zao .

NEW MANDATE:Oparanya Achaguliwa mwenyekiti wa CoG bila kupingwa .

James na mkewe wa miaka zaidi ya 20 walilazimika kutengana baada ya mke huyo kuanza kumpa mateso ya kimawazo kwa kumfanya kelele na pia kuwa na uhusiano wan je ya ndoa na naiu wa chifu na hata afisa mmoja wa polisi . Njenga anasema wakati wa ndoa yake ,wakati mmoja mkewe alitoroka na kumwacha  na mtoto wao aliyekuwa na miezi mitano . Anasema lengo lilikuwa kumfanya aondoke ndiposa mkewe aichukue mali yake .Amesimulia jinsi  kipande chake cha ardhi kilivyozwa na mkewe katika jitihada za  kumwacha mikono mitupu .

PATANISHO: Shiro anataka kumrudia Kamau ‘Mruka mimba’.

Njenga anawashauri wanaume kuwa na ujasiri wa kuweza kusema wazi kwamba wanapitia mahangaiko katika ndoa zao ili waweze kusaidiwa .kwa sasa Bwana Njenga alianzisha shirika lisilo la kiserikali ili kuwapa usaidizi wanaume wanaopitia mateso katika ndoa . Alipoafika mwisho na kuchoka na mateso haya yote  Njenga alioa mke wa pili ambaye wameishi naye kwa miaka tisa sasa bila matatizo .

 

 

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments