Ameumbwa akaumbika! Tazama picha za mtoto wao Diamond na Tanasha Donna

Binti kidosho wa kutoka mumu humu Kenya Bi Tanasha Donna ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamziki stadi Diamond Platnumz.

Wawili hawa walibarikiwa na kitoto kichanga hivi juzi na si siri kuwa wamejawa na furaha tele.

Binti huyu alijifungua kwenye hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam tarehe 2 mwezi wa 10.

  
Kutoka siku hiyo, Tanasha amekuwa akiwaeleza mashabiki wake anavyo jihisi kama mzazi.

Mamake Diamond amekuwa akiweka picha tofauti tofauti za mjukuu wake na kujidai kuwa anafanana naye.

 

  

Tanasha alijifungua kwa njia ya kawaida, yaani hakufanyiwa upasuaji na alipozungumza na mashabiki wake, alisema kuwa atapanga kupata mtoto mwingine baada ya miaka 5.

Vilevile, alifunguka mwanzo mwisho na kusema kuitwa 'mama' ni kitu ambacho kimemfanya awe na furaha sana.