Justice langat

AMEZAA CHAMPION: Mzalishaji Kipindi Justice Langat Ajaliwa Mtoto Akishangilia Riadha Kasarani

Ni habari njema kwa mzalishaji wa Radio Jambo na haswa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi, bwana Justice Langat ambaye pamoja na mkewe walijaliwa, mtoto wa kiume wikendi iliyopita.

Matukio Ya Krismasi Na Justice Langat, 22nd December 2016

Bwana Langat pamoja na mkewe walikuwa wamehudhuria mashindano ya riadha ya wanariadha wasiozidi umri wa miaka kumi na minane, wikendi iliyopita katika ukumbi wa Kasarani na hapo ndipo kijana kwa jina Kiprotich mwenye kilo tatu nukta tano alipobisha hodi duniani.

Mtangazaji Ghost Mulee alikuwa mwingi wa furaha alipokuwa akimsimulia mwenzake Gidi Gidi kuhusu tukio hilo la baraka.

“Langat unajua jana tuliungumza naye, akaniuliza Ghost uko wapi nikamweleza ndio naelekea kasarani. Akanieleza amefika tayari akitazama riadha.” Alisimulia Ghost.

“Sasa baadae kumbe Langat naye akitizama wakati wakenya walikuwa wanashinda katika kitengo cha kuruka viunzi na maji, alikuwa na mkewe ambaye alikuwa mja mzito. Baada ya kushabikia mkewe naye akaanza kuhisi maumivu ya kujifungua, pale pale uwanjani. Uzuri kulikuwa na gari la ambulensi na papo hapo akakimbizwa katika hospitali moja karibu na uga wa Kasarani.

Justice Lang’at and other celebrities who celebrate their birthdays today

Na wamebarikiwa, amezaa mtoto kwa jina Kiprotich aliyezaliwa na kilo tatu nukta tano.” Alizidi kueleza bwana Mulee huku pamoja na Gidi wakiwapongeza baba na mama Kiprotich.

Hongera sana kwa mzalishaji wetu wa vipindi, Justice Langat pamoja na mkewe na tunawatakia furaha na maisha marefu pamoja na mwanao Kiprotich.

Pata usimulizi zaidi katika kanda ifuatayo.

 

Photo Credits: victor TKO imboto

Read More:

Comments

comments