logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bashasha huku mahasidi Diamond na Harmonize wakikutana na kufurahia pamoja

Diamond na Harmonize, mnamo Jumanne jioni walipata fursa adimu ya kuwa kwenye ukumbi mmoja baada ya muda mrefu sana.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani14 March 2024 - 04:30

Muhtasari


  • •Diamond na Harmonize, mnamo Jumanne jioni walipata fursa adimu ya kuwa kwenye ukumbi mmoja baada ya muda mrefu sana.
  • •Wawili hao waliokuwa wamevalia mavazi yanayoenda kufanana walionekana kufurahi sana kukutana na wakafanya mazungumzo yasiyosikika.

Mastaa wawili wa bongofleva, Diamond Platnumz na Harmonize, mnamo Jumanne jioni walipata fursa adimu ya kuwa kwenye ukumbi mmoja baada ya muda mrefu sana.

Wawili hao wanaoaminika kuwa wapinzani wakubwa katika tasnia ya muziki wa bongo fleva walikutana na hata kusalimiana katika Ikulu ya Tanzania wakati wa sherehe za Iftar iliyoandaliwa na rais Samia Suluhu Hassan.

Mburudishaji Mwijaku alishiriki picha na video za mkutano wao mzuri, na akajipiga kifua kuwa aliwafanya wakutane.

"Nguvu ya mama imeonekana leo, Samia Suluhu Hassan!! Leo nimewakutanisha Diamond Platnumz na Harmonize, nikasema hakuna ninachoweza kushinda!!," Mwijaku alijigamba.

Katika moja ya video alizoshiriki mburudishaji huyo, Harmonize alionekana akimsalimia aliyekuwa bosi wake Diamond ambaye alikuwa amekaa chini.

Wawili hao ambao walikuwa wamevalia kanzu nzuri zinazoenda kufanana walionekana kufurahi sana kukutana na wakafanya mazungumzo yasiyosikika.

“Nguvu ya Mama haina mpinzani, Samia Suluhu Hassan amenipa maagizo na nimeyatekeleza! Watu muhimu sana! Diamond Platnumz na Harmonize tayari wameshapeana mikono hapa Ikulu,” aliandika Mwijaku chini ya video hiyo.

Pia alishiriki picha zaidi za mastaa hao wawili wakubwa wa bongo pamoja na watu wengine mashuhuri kwenye ikulu ya serikali.

Mshindani mwingine wa Diamond, Alikiba pia alikuwepo katika ikulu wakati wa hafla hiyo lakini haijafahamika iwapo wao pia walipata kukutana na kuzungumza

Jux, Maua Sama na mchekeshaji Joti ni miongoni mwa mastaa wengine waliohudhuria sherehe hizo.

Mashabiki wameendelea kusherehekea na kupongeza mkutano baina ya Diamond na Harmonize na kuwasihi wamalize uhasama na kudumisha uhusiano mzuri.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved