In Summary

•Alipuuzilia mbali kutengana kwa sababu ya kutokuwa na uaminifu akibainisha kuwa watu walio karibu nao wamesababisha kuvunjika kwa mahusiano yao.

•"Sasa tumegundua kuwa hatuwezi kuishi bila kila mmoja, na uhusiano wetu ni mkubwa sana kuweza kutengana," alisema.

Akothee na mpenziwe Nelly Oaks.
Image: FACEBOOK// AKOTHEE

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri wa Kenya Esther Akoth almaarufu Akothee amefichua wazi kwamba amekuwa kwenye uhusiano na meneja wake Nelly Oaks kwa takriban mwongo mmoja.

Katika chapisho la Jumanne jioni, msanii huyo mwenye umri wa miaka 43 alifichua kuwa katika uhusiano wake wa miaka 10 na mpenziwe huyo ambaye jina lake halisi ni Nelson Oyugi, wameachana mara mbili.

Hata hivyo alipuuzilia mbali tuhuma za kutengana kwa sababu ya kutokuwa na uaminifu akibainisha kuwa watu walio karibu nao wamesababisha kuvunjika kwa mahusiano yao.

"Mimi na Nelly tumeachana mara mbili katika uhusiano wetu wa miaka 10, lakini hatukuwahi kuwa na matusi kwenye mitandao ya kijamii. Kuachana kwetu kwa mara ya mwisho kulikuwa kugumu, lakini haikutokana na ku’cheat hatukuwahi kuwa na masuala ya kukosa uaminifu.

Badala yake, matatizo yetu mengi yametokana na watu tunaowaruhusu kwenye miduara yetu. Kuachana kwetu kwa kawaida hutokea tunapokuwa mbali na kila mmoja kwa muda mrefu sana,” Akothee alisema kupitia mtandao wa Facebook.

Mama huyo wa watoto watano alisema kuwa yeye na Nelly Oaks sasa tayariwamekubali kwamba wanahitaji kila mmoja ili kuishi.

Pia alifichua kuwa walirudiana bila masharti na bila kuhusisha watu wengine.

"Sasa tumegundua kuwa hatuwezi kuishi bila kila mmoja, na uhusiano wetu ni mkubwa sana kuweza kutengana. Wakati tuliotengana, sote tulikosana sana. Tulipopatana, hatukuuliza chochote au mtu yeyote tulirudi tu na nguvu zaidi kuliko hapo awali, "alisema.

Aliongeza, "Upatanisho ni rahisi zaidi wakati suala linabaki kati yenu wawili. Mara tu unapohusisha umma, inakuwa vigumu zaidi kuelekeza. NAMPENDA MTU WANGU HADI KIFO.”

Haya yanajiri katika wakati ambapo mwimbaji huyo tayari amedokeza kuhusu harusi kubwa ambapo anatarajiwa kufunga pingu za maisha na mpenzi huyo ambaye pia ni meneja wake.

View Comments