In Summary

•Mwanasosholaiti huyo alikuwa na marafiki zake alipoweka wazi kuwa hawezi kuwa kwenye uhusiano ambapo ataishi mbali na mpenzi wake.

•“Mimi nataka mambo ya kweli. Hizi mambo zao siwezi. Nataka kuona, nataka kufeel,” alisema.

Amber Ray
Image: HISANI

Katika kipande kidogo cha video ya filamu ya maisha halisia ya Nai-Rich ambayo yeye na mumewe ni sehemu yake, mwanasosholaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray alizungumza kuhusu maoni yake kuhusu uhusiano wa masafa marefu.

Mwanasosholaiti huyo alikuwa kwenye meza ya chakula pamoja na marafiki zake ambao baadhi pia ni sehemu ya waigizaji alipoweka wazi kuwa hawezi kuwa kwenye uhusiano ambapo ataishi mbali na mpenzi wake.

Amber Ray alieleza kuwa anahitaji kuwa na mwanaume wake sana na akadokeza kuwa hayuko tayari kutumia vinyago ili kujiridhisha kimapenzi.

"Mahusiano ya mbali haiwezi kufanya kazi. Aje? Mimi ni Mkamba? Aje? Eti vinyago, vinyago ni baridi, sijui betri zimeisha..,” Amber Ray alisema.

Sosholaiti huyo alifichua kwamba katika siku za nyuma amekuwa kwenye uhusiano wa umbali mrefu ambapo angeshiriki katika mawasiliano ya video na mpenzi wake. Hata hivyo, anasema hakufurahishwa na hali hiyo kwani anataka mwanaume wake awe karibu naye kila mara.

“Mimi nataka mambo ya kweli. Hizi mambo zao siwezi. Nataka kuona, nataka kufeel,” alisema.

Aliongeza, “Ukipanda ndege eti long-distance, wewe beba roho yako ukiendaga, usiniachie.

Mwanasholaiti huyo kwa sasa ameolewa na mfanyabiashara tajiri Kennedy Rapudo na wawili hao tayari wamejaliwa kupata mtoto pamoja.

Hapo awali alikuwa ameolewa na mjasiriamali Jimal Marlow Rohosafi kabla ya kutengana takriban miaka mitatu iliyopita.

View Comments