In Summary

• Alisisitiza kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu mkewe kuchukua mkopo kwa kutumia nyumba yake na wala hakuwahi kuitwa mahakamani wakati mkopo huo ulichelewa kulipwa.

JAMAA ALIA MKEWE KUUZA NYUMBA.
Image: HISANI

Mwanamume mmoja amechukua mafadhaiko yake katika mtandao wa X na kuonyesha jinsi alivamiwa nyumbani na watu kutoka kwa benki kwa nia ya kupiga nyumba yake mnada.

Katika video hiyo ambayo mwanamume huyo alichapisha kwenye X, alirekodi jinsi watu hao kutoka benki waliwasili nyumbani kwake wakiandamana na polisi kwa lengo la kuitwaa nyumba yake bila yeye kujua.

Alipouliza, watu hao walimwambia kwamba mkewe alitumia nyumba hiyo kama dhamani kuchukua mkopo benkini na baada ya kushindwa kurudisha mkopo, waliamua kuja na kuipiga mali yake mnada.

‘Niko LIVE kutoka nyumbani kwangu, acha dunia nzima ishuhudie. Wanasema mke wangu alichukua mkopo kutoka benki ambayo sijui na sasa wametuma watu kuja kunitupa nje. Naapa nitakufa,” mwanamume huyo alisema.

Alisisitiza kwamba hakuwa na taarifa yoyote kuhusu mkewe kuchukua mkopo kwa kutumia nyumba yake na wala hakuwahi kuitwa mahakamani wakati mkopo huo ulichelewa kulipwa.

“Sijawahi itwa kortini kuambiwa nyumba yake inataka kupigwa mnada, alitumia mali yangu kama dhamana na sasa wamekuja kutupa vitu vyangu nje,” mwanamume huyo aliongeza huku akitembea na kamera kwenda ndani ya jumba hilo.

Alieleza kwamba mkewe alianza kuondoka nyumbani na bidhaa moja baada ya kingine bila kumuambia chochote.

Tazama video hiyo hapa;

 

View Comments