In Summary

• Hamo alisema kwamba babake rafiki yake ambaye aligunduliwa kuwa na saratani ya koo alihitaji damu O-  lakini walikuwa wameikosa na Nyahururu, Gilgil na Naivasha.

Profesa Hamo
Image: Instagram

Mchekeshaji Herman Kago almaarufu Prof Hamo amewatahadharisha wakenya dhidi ya matapeli wanaojifanya madaktari.

Kupitia video aliyopakia kwenye Instagram siku ya Jumatano, Hamo alisimulia jinsi mgonjwa wa saratani alivyoibiwa  shilingi 18,000 baada ya mtu mmoja alijifanya daktari kumlaghai pesa hizo akiwa hospitalini.

Hamo alisema kwamba babake rafiki yake ambaye aligunduliwa kuwa na saratani ya koo alihitaji damu O-  lakini walikuwa wameikosa na Nyahururu, Gilgil na Naivasha.

Siku ya Jumapili , rafiki yangu akaniambia babake aliyekuwa amepatikana  na saratani ya koo anahitaji damu aina ya O-, na the whole of Nyahururu, Gilgil, Naivasha walikuwa wamekosa."

Alitumiwa maelezo na yeye akazichapisha kwa mtandao na baadaye alipigiwa simu na rafiki yake akimshukuru kwa sababu watu walikuwa wamejitokeza.

"So akanitumia details and I just posted here. Nikaiweka hapo kwa mtandao. So jana she texted me akaniambia ‘eeh manze thank you so much tumepata wasee. Wasee wamenicall wengine wamekam through'."

Jumatano alitumiwa ujumbe na kuambiwa kuwa kuna mtu ambaye alienda hospitalini na kujifanya daktari. Tapeli huyo huyo alikwenda kwa chumba cha mgonjwa na kujitambulisha kama daktari Mungai. Alifaulu kupata Ksh.18,000 kutoka kwa mgonjwa baada ya kusema kuwa anajua mahali wanaweza pata damu kwa bei nafuu.

"Today napata text akaniambia walikuja na wengine wakakuja mpaka wezi...Apparently someone showed up akaenda hosi alafu akakuta some of the people who are care givers hapo kwa hosi hawakuwa kwa ward so he went straight to the bed there ya mzae akajiintroduce as a doctor. Dr Mungai. Akaambia mzae there is a medication alikuwa anataka kutry and you know because it’s a public hospital so you don’t know, madaktari ni wengi so this guy said he knows wapi tunaeza ipata cheaply...So mzae akamuuliza how much?...akamtumia 18,000. Mse akachukua 18K na akaondokea."

Walijaribu kumpigia daktari Mungai simu lakini hawakufaulu kumpata. Kago alisema kuwa kwa sasa mshukiwa anatafutwa na hivi  karibuni atashikwa.

"Kumbe walitry kumcall and they couldn’t get him. But now she has talked to some people anatrakiwa down...very soon atakuwa ameshikwa. Can you imagine the audacity,yaani we don’t care...unaibia mgonjwa...Dr Mungai we are looking for you we’ll find you. Dawa utatoa, na pia sisi tutakupea dawa.”

Amewashukuru wale ambao walisambaza ujumbe na kusema kuwa hatimaye mgonjwa anapata matibabu.

"But thank you everyone who circulated that message. Finally mzae amepata dawa, amepata O- and we are glad .Treatment zinaendelea poa." alisema.

View Comments