In Summary

•Wawili hao walitangaza habari za kusisimua za ujauzito wa mtoto wao wa pamoja kupitia video ya kupendeza ambayo alichapisha Alhamisi jioni.

•Ujauzito mkubwa ambao amebeba unaweza kuonekana kwenye video.

Image: HISANI

Wanandoa mashuhuri Peter Kabi na Millicent Wambui wa familia ya The Wajesus wanatarajia mtoto wao wa tatu hivi karibuni.

Wawili hao walitangaza habari za kusisimua za ujauzito wa mtoto wao wa pamoja kupitia video ya kupendeza ambayo alichapisha Alhamisi jioni.

Katika video hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa YouTube, Milly alionekana akikimbia kwenye mtaa mmoja mzuri katika jiji la Dubai kabla ya kusimama kwa ajili ya picha ya pamoja na mumewe Kabi. Ujauzito mkubwa ambao amebeba unaweza kuonekana kwenye video.

“Tazama Bwana amefanya nini!! Miaka 7 iliyopita tulienda Dubai kwa honeymoon na miaka 7 baadaye tumerudi kutangaza ujauzito wa mtoto wetu wa tatu!! Asichoweza Mungu hakipo!!,” Kabi alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande wake, Milly alibainisha kwamba mimba ya mtoto wake wa tatu ni sala iliyojibiwa.

“Ya kusisimua ni taarifa isiyotosha!! Mungu ametutabasamia tena. Tuliomba kwa ajili ya mzaliwa wa tatu na kwa wakati wake kamili, alijibu maombi yetu. Mtoto nambari 3 akipakia timu mvulana au msichana,” alisema.

Wanamitandao wengi wakiwemo mastaa wenzao wameendelea kumwaga jumbe za pongezi kwa wanandoa hao na kuwatakia kila la heri wakati wakimsubiri mtoto wao wa tatu.

Kabi na Milly tayari wana watoto wawili pamoja, mvulana mmoja na msichana  mdogo ambaye alizaliwa takriban miaka miwili iliyopita.

Mtoto wao wa kwanza, Reign Taji ana umri wa miaka mitano huku mtoto wa pili  Princess Tsuri Wa Jesus akiwa na umri wa miaka miwili.

View Comments