In Summary

• Rappa Young Thug amejiunga na wasanii wengine kunyooshea kidole cha lawana ubaguzi wa rangi katika mzozo wa kivita unaondelea nchini Ukraine.

Beyonce, Young Thug
Image: Instagram

Watu wenye uwezo na wahisani mbalimbali wametangaza kujitolea ili kutoa misaada yao kwa wahanga wa vita vya Ukraine na Urusi ambao wamekwama nchini Ukraine baada ya majeshi ya Urusi kuingia huko na kuanza mashambulizi.

Mzozo nchini Ukraine umeendelea kwqa wiki moja sasa huku watuwakijaribu kutorokea maeneo salama kama kuingia mataifa Jirani ya Poland, ambapo pia video zimesambazwa mitandaoni zikionesha visa vingine vya ubaguzi wa rangi haswa kwqa watu wenye rangi nyeusi ya Ngozi wanaozuiliwa kutoroka nchini Ukraine huku wengine wakilazimishwa kuachia nafasi zao za viti katika magari ili Waukraine kuzitumia.

Tukio hilo limekashfiwa sana kote duniani huku sasa watu mbalimbali wakijitolea kutoa misaada yao ili kuwasaidia Wafrika waliokwama kwenye maeneo ya mipaka ya Ukraine kukimbilia maeneo salama.

Wa hivi punde kutangaza kutoa msaada wao ni msanii Young Thug ambaye kupitia Instagram yake ameandika kwamba kama kuna mtu ambaye ni ndugu yake wa rap basi ako ange kutoa msaada ili kuona kwamba wako salama.

“Kama kuna mtu ambaye ni ndugu yangu wa rap, basi niko tayari kusaidia Wafrika kutoka nje ya Ukraine hata kama ninahisi hawataturuhusu tupite,” aliandika Young Thug.

Awali msanii Beyonce kupitia kwa wakfu wake wa Bey Good walisema kwamba wameshtushwa na vitendo vinavyoendelea dhidi ya watu Weusi wanaozuiliwa kuondoa Ukraine lakini wanaendelea kutafuta njia za kuwasaidia kwenda maeneo salama.

Wasanii wengine ambao pia wametoa jumbe zao za kusimama upande wa Faraja ya watu wa Ngozi nyeusi ni Card B, Gunna miongoni mwa wengine.

Haya yanakuja saa chache tu baada ya klabu yqa mpira wa miguu ya Chelsea kutoa taarifa kwamba mmiliki wa timu hiyo Roman Abrahamovic anapanga kuuza klabu hiyo na malimbikizi yake kutumika kuwasaidia wahanga wa vita hivyo nchini Ukraine.

View Comments