In Summary

• Kulingana na nakala ya Jarida la Forbes, bidhaa hiyo ilivutia watu wengi katika mnada wa mtandaoni kufuatia urushaji maikrofoni.

Card B.
Image: Screengrab

Kipaza sauti ambacho msanii wa Marekani Card B alidaiwa kumtupia shabiki mmoja na kumjeruhi nacho mwishoni mwa mwezi Julai kimeripitiwa kupigwa mnada kwa kima cha takribani shilingi milioni 14 pesa za Kenya [$99000].

Kwa mujibu wa taarifa mbali mbali, maikrofoni hiyo iliwekwa sokoni na watu mbali mbali wakawasilisha dau la kutaka kukinunua ili kuwa kweney historia ya kumiliki kipaza sauti hicho.

Kufikia Jumanne, ilidaiwa kwamba mtu mmoja alikuwa ametoa dau la kiasi hicho cha pesa kwenye mtandao wa mauzo ya kidijitali, e-Bay ili kukinunua.

Kulingana na nakala ya Jarida la Forbes, bidhaa hiyo ilivutia watu wengi katika mnada wa mtandaoni kufuatia urushaji maikrofoni uliotangazwa sana. Maikrofoni ilivutia zaidi ya zabuni 120 kabla ya kuuzwa.

Mnamo Julai 29, wakati akitumbuiza katika Klabu ya Ufukweni ya Drai’s huko Las Vegas, mshiriki mmoja wa watazamaji alimrushia kinywaji rapper huyo ambaye alijibu kwa kurusha kipaza sauti chake kwenye watazamaji.

Inasemekana kipaza sauti kilimpiga mwanamke ambaye aliwasilisha ripoti ya polisi. Cardi B baadaye aliorodheshwa kama mshukiwa wa kesi ya kuzua rabsha kwenye tafrija.

Uchunguzi wa jinai ulizinduliwa kuhusu tukio hilo lakini baadaye ukatupiliwa mbali kwa sababu ya ushahidi wa kutosha.

Video za sakata ya kurusha maikrofoni zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na ilidaiwa kwamba Cardi B ndiye aliwataka mashabiki wake kumrushia maji ya chupa wakati anatumbuiza jukwaani.

View Comments