In Summary

• Katika hali mpya, shabiki aliuliza, "Je, idadi ya mwili wako ni ngapi?" ambayo Kizz Daniel alijibu kwa urahisi, “67″.

KIZZ DANIEL
Image: X

Mkali wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria, Oluwatobiloba Daniel Anidugbe, maarufu kama Kizz Daniel amefichua idadi ya wanawake aliolala nao kwa miaka mingi.

Wakati wa kipindi chake cha hivi majuzi cha maingiliano na mashabiki wake kupitia programu ya X siku ya Jumamosi, mwimbaji huyo wa ‘Buga’ alifichua kuwa amefanya mapenzi na wanawake 67 tofauti.

Inaweza kukumbukwa kwamba Kizz Daniel hivi majuzi alifichua kwamba anatengeneza N285 milioni kila siku kama mwanamuziki, na hivyo kuzua hisia nyingi kwenye mtandao.

Katika hali mpya, shabiki aliuliza, "Je, body count yako ni ngapi?" ambayo Kizz Daniel alijibu kwa urahisi, “67″.

Msanii huyo anayetajwa kuwa wa kipekee ambaye hajawahi toa muziki mbaya tangu aingie kwenye Sanaa amekuwa na mazoea ya kuyajibu maswali mbalimbali ya mashabiki wake kwenye mtandao wa X.

Itakumbukwa wakati wa michuano ya Afcon, alimuahidi shabiki mmoja kumpeleka nchini Uingereza iwapo ubashiri wa shabiki huyo kwamba Nigeria ingeibandua Afrika Kusini kwenye nusu fainali ungetimia.

Na kweli kwa maneno yake, baada ya Nigeria kuibandua Afrika Kusini kupitia matuta ya penati, Kizz Daniel alirudi kwenye mtandao huo na kumkumbusha shabiki huyo kwamba anafaa kujiweka tayari kwa kutafuta visa kwa ajili ya safari yake.

Kizz Daniel alisema atamsafirisha shabiki huyo pamoja na timu yake kuelekea kwenye shoo yake kubwa nchini Uingereza mwezi Aprili mwaka huu.

View Comments