In Summary

• Alipoulizwa kuhusu yeye na Babushka kuchumbiana alisema kuwa walikuwa wanafanya tangazo la biashara ya hoteli na hawako katika uhusiano wowote.

•Ameweza kupata tuzo tofauti tofauti ikiwemo Next Generation Influencer of the year

Kate Thuku
Image: HISANI

Mburudishaji Kate Thuku, amesema kwamba hana sababu mbona  ako single.

Katika mahojiano na Oga Obinna, Thuku alisema kuwa yuko soko na hana sababu ya kwanini yeye yuko single.

“Niko soko very bad...I don’t have a reason as to why I’m single…Hakuna mtu amekuja kwangu nikampea standards akajitoa,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu yeye na Babushka kuchumbiana alisema kuwa walikuwa wanafanya tangazo la biashara ya hoteli na hawako katika uhusiano wowote.

“Hebu nikuambie kilichokuwa kikiendelea huko ili kunyoosha maelezo. Kuna ile hoteli tuliyokuwa , tulikuwa tunaitangaza hoteli hiyo. Tulikuwa tunafanya tangazo tu, tangazo la kawaida,” alisema.

Kate pia aliongeza kuwa hawezi kuchumbiana na mwanamume ambaye hana pesa.

“Kusema kweli nisingesema, mi nasema tu ukweli. Akuwe tu stable, kuna tofauti kati ya broke, stable and rich rich. Nisingeolewa na mwanamume fukara ni afadhali kuolewa na mwanamume mwenye uwezo.”

Kate ni mtayarishaji maudhui ambaye ameweza kupata tuzo tofauti tofauti ikiwemo Next Generation Influencer of the Year, Video Vixen of the Year.


View Comments