In Summary

• Hivi majuzi, Salasya alidokeza kwamba ana nia kuu ya kuanzisha familia mwaka ujao, akiweka wazi lengo lake la kuoa wanawake wasiopungua idadi ya 3.

SALASYA
Image: FACEBOOK

Mbunge wa Mumias Mashariki, Peter Salasya  amesema moja kati ya ndoto yake kuu pindi atakapoanza kuwa mzazi ni kuona wanawe wakiwa wasomi.

Akizungumza kupitia chaneli yake ya YouTube, Salasya alisema kwamba angependa kuona wanawe, haswa mabinti wakisoma na kutafuta pesa zao wenyewe kwa kutumia akili.

Mbunge huyo alisema kwamba anawaheshimu sana wanawake na anajua kuwa maisha ni magumu haswa kwa kina dada ambao hawatumii akili kutafuta riziki, kwani nyeti zao hubeba lawama zote.

“Mimi ningependa kusema kwamba nawahehsimu sana wanawake. Wanawake ni watu wa ajabu sana, na kusema kweli mimi wakati nitaanza kuzaa, nataka watoto wangu wasome, na watumie akili, wajue kutafuta pesa zao wenyewe,” alisema.

“Kwa sababu sasa hivi maisha ni magumu, na wanasema kwamba kama kama huna akili nyeti zao huumia pakubwa na huo ndio ukweli. Mimi nisingependa kuwaona mabinti zangu wakiumia, bali watumie akili kutengeneza pesa zao wenyewe na si kuishi maisha ya kuigiza,” Salasya aliongeza.

Kauli hizi zilijiri muda mfupi baada ya kutupiana makovu na mwanasosholaiti Huddah Monroe katika mitandao ya kijamii baada ya kile kilichoonekana kuwa ni kusambaratika kwa mapenzi yao ambayo ndio yalikuwa katika hatua za mwanzo mwanzo.

Hivi majuzi, Salasya alidokeza kwamba ana nia kuu ya kuanzisha familia mwaka ujao, akiweka wazi lengo lake la kuoa wanawake wasiopungua idadi ya 3.

View Comments