In Summary

• Eve Mungai anasema kuwa katika uhusiano wake wa sasa ana matumaini ya kupelekewa mahari

• Trevor na Eve waliachana mwezi Februari mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa takribani miaka 6

MUNGAI EVE
Image: Instagram

Mtayarishaji maudhui Eve Mungai anasema kuwa katika uhusiano wake wa sasa ana matumaini ya kupelekewa mahari .

Akiwahoji Nebz na Nyathira, alifichua kwamba kwa mwaka mmoja alikuwa tayari ashajua uhusiano wake wa zamani haungefika mbali.

I was ready. I was actually ready for a year plus,"

Katika uhusiano wake mpya ambao bado hajaweka wazi, alisema kuwa uhusiano wao unakaribia kuadhimisha mwaka wa kwanza.

"Mimi sahii naenda kumaliza mwaka mmoja. Mimi huwa nipo kwenye mahusiano by the time namalizana huku, najua the next. Mambo ya social media wachana nayo...Hii iko na potential,"

Pia alisema kuwa mwaka huu umekuwa mwaka mzuri kwake kimwili na kifedha haswa kifedha.

"Kwa kweli mwaka huu umekuwa mwaka wangu bora zaidi. kifedha, kiakili. Hasa kifedha,"

Kuhusu uhusiano wake wa sasa alisema kuwa anamatumaini atapelekewa mahari na sio kama uhusiano yake ya awali.

"Sahizi, mahali niko naona nitapelekewa [mahari]. Pale pengine naona nikama ni mimi ndio ningejitolea,"

Trevor na Eve waliachana mwezi Februari mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa takribani miaka 6.


View Comments