In Summary

• Katika video hiyo ambayo ilizua mjadala pevu mitandaoni, Mama Dangote alikuwa ameketi kwenye meza akiwa ameshikilia chupa ya maji yenye chapa ya kampuni.

MAMA DANGOTE
Image: Instagram

Hatimaye, Mama Dangote amefunguka kuhusu sababu iliyompelekea kutupa chupa ya maji yenye chapa ya kampuni husika chini ya viti baada ya kumuona Diamond.

Katika video hiyo ambayo ilizua mjadala pevu mitandaoni, Mama Dangote alikuwa ameketi kwenye meza akiwa ameshikilia chupa ya maji yenye chapa ya kampuni.

Ghafla, Diamond aliingia akiwa ameandamana na wapiga picha na mamake alionekana kuchanganyikiwa kabla ya kuitupa chupa hiyo chini ya kiti katika kile kilichoonekana kama kuificha mbali na wapiga picha.

Baadae alifunguka kuhusu tukio hilo na kusema kwamba hakuwa anataka kuipa promo kampuni ambayo Diamond hana mkataba wa matangazo ya kibiashara nayo ndio maana akaificha chapa hiyo mbali na kamera.

“Naona watu wamenivamia, naona wanakuja na kamera, na mimi nikawahi kuitupa hiyo chupa isionekane chapa. Lengo lilikuwa kuificha chapa isionekane kwa sababu siwezi kuipa promo kampuni ambayo mwanangu hana mkataba nao,” Mama Dangote alisema.

Alisisitiza kwamba tukio hilo si geni kwake kwani mara kwa mara anapotumia bidhaa zenye chapa ambazo mwanawe hana mkataba wa matangazo ya kibiashara nao, huwa anajitahidi sana kuficha lebo isionekane.

“Si mara ya kwanza, wewe niangalie wakati ambapo ninatumia vitu, kwa mfano nakunywa soda lazima nikunywe yenye mkataba wa matangazo ya kibiashara na Diamond, kama ninakunywa maji ya kawaida, lazima nichune na kutupa karatasi yenye chapa. Kwa sababu sitaki kutoa promo ya bure kwa kampuni isiyo na mkataba na mwanangu. Nimeshazoea hivyo,” Mama Dangote alieleza zaidi.

View Comments